• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mbwa wa polisi atimuka na mpira uwanjani

    (GMT+08:00) 2017-11-02 08:45:55

    Mbwa wa polisi amezua taharuki wakati alipoingia uwanjani na kukimbia na mpira kwenye mchezo kati ya Blooming dhidi ya Nacional de Potosi wa Ligi Kuu ya Bolivia. Mbwa huyo wa polisi alifanikiwa kutoka mikononi mwa askari aliyekuwa amemshika na kuingia uwanjani wakati mechi ikiendelea kabla ya kuung'ata mpira na kukimbia nao. Kitendo hicho cha mbwa kukimbia na mpira ukiwa mdomoni mwake kilisababisha mechi kusimama kwa sekunde 40. Askari walianza kumkimbiza mbwa huyo uwanjani jambo lililofanya mashabiki na watazamaji kupata burudani ya aina yake. Mwisho mchezaji Alejandro Quintana anayechezea Blooming alifanikiwa kumkata mbwa huyo na mechi kuendelea. Hadi mchezo unamalizika Blooming ikaongoza kwa mabao 4-2, lakini mbwa huyo wa polisi ndiye aliyeshika vichwa vya habari.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako