• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Iraq yalishutumu jeshi la wakurdi kukiuka makubaliano ya kuweka vikosi vya jeshi la taifa

    (GMT+08:00) 2017-11-02 09:33:48

    Kituo cha operesheni za pamoja cha Iraq kimelishutumu jeshi la wakurdi kukiuka makubaliano kati yake na jeshi la taifa la Iraq kupanga majeshi ya serikali kwenye maeneo yanayogombewa na vituo vya kuvuka mpaka.

    Taarifa iliyotolewa na kamati hiyo imesema viongozi wa jimbo la wakurdi na kikundi chao cha majadiliano wameikana rasimu ya makubaliano waliyofikia na kikundi cha serikali kuu. Hatua hiyo inachukuliwa kama ni mbinu ya majadiliano, ambayo itawarudisha nyuma kwenye mwanzo wa mazungumzo.

    Taarifa pia imesema katika kipindi cha mazungumzo wakurdi walihamisha vikosi vyao na kuunda mistari mipya ya ulinzi, ili kukwamisha upangaji wa vikosi vya serikali kuu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako