• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Russia yawaalika wapinzani wa Syria kuhudhuria mkutano wa majadiliano ya kitaifa

    (GMT+08:00) 2017-11-02 09:34:07

    Russia imeyaalika makundi 33 ya upinzani kuhudhuria mkutano wa baraza la majadiliano ya kitaifa uliopangwa kufanyika katika mji wa Sochi baada ya mwezi mmoja.

    Mkutano huo unatarajiwa kuunga mkono uwezekano wa kufanya mazungumzo kati ya serikali ya Syria na makundi ya upinzani kabla ya raundi nyingine ya mazungumzo ya Geneva kuhusu mgogoro wa Syria yanayotarajiwa kufanyika Novemba 28.

    Baadhi ya wachambuzi wamepongeza uamuzi wa Russia kwa kusema ni hatua nzuri ya kufanya kuwe na mtazamo wa pamoja kwenye majadiliano ya utatuzi wa mgogoro wa Syria, ikiwa ni pamoja na majadiliano kuhusu katiba mpya ya Syria.

    Hata hivyo baadhi ya makundi yamepinga na kukataa kushiriki kwenye mkutano huo. Kundi la Syria National Coalition lenye makao yake nchini Uturuki limesema mkutano huo ni mbinu ya Russia kukwepa mazungumzo ya Geneva.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako