• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Marekani kufanya ziara ya kitaifa nchini China

    (GMT+08:00) 2017-11-02 09:37:49

    Msemaji wa Wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Lu Kang ametangaza kuwa, kutokana na mwaliko wa rais Xi Jinping, rais Donald Trump wa Marekani atafanya ziara ya kitaifa nchini China kuanzia tarehe 8 hadi 10 Novemba.

    Kwenye ziara hiyo, viongozi hao wawili watabadilishana maoni kuhusu uhusiano kati ya China na Marekani na masuala muhimu ya kimataifa na ya kikanda wanayoyafuatilia kwa pamoja. Amesema China inapenda kushirikiana na Marekani, kufanikisha mkutano wa marais wa nchi mbili, ili kuingiza msukumo mpya kwenye maendeleo ya uhusiano kati ya pande hizo mbili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako