• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tume ya Umoja wa Mataifa kupanua majukumu yake nchini Sudan Kusini

    (GMT+08:00) 2017-11-02 09:43:12

    Tume ya Umoja wa Mataifa inapanga kupanua majukumu yake nchini Sudan Kusini ili kukiwezesha kikosi chake cha kulinda amani kuwasaidia watu wengi zaidi walio hatarini katika maeneo ya mbali nchini humo.

    Mkuu wa tume ya kulinda amani ya Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini UNMISS, Bw David Shearer amesema kuwafika watu walio hatarini katika maeneo ya mbali nchini humo, ni mbinu nyepesi na yenye ufanisi ya tume hiyo.

    Bw. Shearer amesema hayo katika mji wa Akobo karibu na mpaka wa Ethiopia. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na UNMISS, wakimbizi wa ndani wapatao elfu 71, wanaishi Akobo na maeneo ya karibu, baada ya kukimbia mapambano kati ya kundi la SPLA na kikosi cha upinzani kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako