• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • CAF yatangaza orodha ya wachezaji 30 watakaowania taji la mchezaji bora wa soka barani Afrika mwaka huu.

    (GMT+08:00) 2017-11-02 10:14:45

    Shirikisho la soka barani Afrika limetoa orodha ya wachezaji 30 watakaowania taji la mchezaji bora wa soka barani Afrika mwaka huu. Mshambuliaji wa Gabon Pierre Erick Aubameyang aliyeshinda mwaka 2015 ameorodheshwa pamoja na nyota kadhaa wanaosakata dimba barani Ulaya kama vile mshambuliaji wa Senegal na Liverpool Sadio Mane ambaye alikuwa katika nafasi ya tatu 2016. Mshindi wa mwaka 2016 Riyad Mahrez wa Algeria hakuorodheshwa katika orodha hiyo. Kati ya wachezaji 30 waliorodheshwa ni saba pekee ambao hawachezi soka yao barani Ulaya, huku kipa wa Misri aliye na umri wa miaka 44 pia akiorodheshwa. Wachezaji wanne wanaosakata soka yao Afrika wameorodheshwa kuwania taji la mchezaji bora wa bara Afrika mbali na mchezaji bora anayesakata soka barani humu. Washindi wa mataji hayo watatangazwa katika mji mkuu wa Ghana Accra mnamo tarehe 4 mwezi January 2018.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako