• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Riadha: Shirikisho la Riadha Tanzania latangaza wanariadha 19 watakaoshiriki michuano ya Jumuiya ya Madola Australia

    (GMT+08:00) 2017-11-02 10:15:08

    Shirikisho la Riadha Tanzania (RT) limetangaza idadi ya wanariadha 19 watakaoingia kambini mapema mwezi huu Lushoto mkoani Tanga kusaka pumzi kwa ajili ya michuano ya Jumuiya ya Madola itakayofanyika Australia Aprili mwakani. Katibu Mkuu wa RT Wilhelm Gidabuday alisema wanariadha 10 tayari wameshafuzu na wengine tisa wametafutiwa mashindano kwaajili ya kwenda kusaka viwango vinavyotakiwa kwenye mashindano hayo kabla ya Januari mwaka ujao. Wakati huohuo mkimbiaji wa Afrika Kusini Wayde van Niekerk ataikosa michuano hiyo baada ya kuumia goti wakati akishangilia. Van Niekerk bingwa wa michuano ya mita 400 ya dunia na michuano ya Olimpiki alikuwa na nia ya kushiriki michuano ya mita 100 na 200 nchini Australia. Kwa sasa atahitaji kufanyiwa upasuaji ili kuweza kuwa fiti kuendelea na michuano mingine. Michuano ijayo ya Jumuiya ya Madola itafanyika April 4 mpaka 15 katika mji wa Gold Coast nchini Australia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako