• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Maonesho ya kwanza ya kimataifa ya bidhaa za nchi za nje kufanyika mjini Shanghai

    (GMT+08:00) 2017-11-02 17:33:13

    Maonesho ya kwanza ya kimataifa ya bidhaa za nje yatafanyika kuanzia tarehe 5 hadi 10, mwezi Oktoba mwaka kesho mjini Shanghai, China, na yanatarajiwa kuhudhuriwa na kampuni kutoka nchi na sehemu zaidi ya 100 duniani.

    Kwenye mkutano wa kilele wa ushirikiano kimataifa kuhusu "ukanda mmoja, njia moja" uliofanyika mwezi Mei mwaka huu mjini Beijing, rais Xi Jinping wa China alitangaza kuwa China itaandaa maonesho ya kimataifa ya bidhaa za nchi za nje kuanzia mwaka 2018. Naibu waziri wa biashara wa China, ambaye pia ni mwakilishi wa China katika mazungumzo ya biashara za kimataifa Bw. Fu Ziying, kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika jana alisema, maonesho ya kwanza ya kimataifa ya bidhaa za nje yatakuwa na eneo la mita laki 2.4 za mraba, na kugawanywa katika maonesho ya biashara na uwekezaji wa nchi, pamoja na maonesho ya biashara za kampuni. Bw. Fu Anasema,

    "Madhumuni ya kuandaa maonesho ya biashara na uwekezaji wa nchi ni kuzipatia nchi zenye hali tofauti za uchumi jukwaa la kuongeza ushawishi, na kukuza ushirikiano wa biashara za kimataifa. Kwenye maonesho hayo, nchi zinazohusika zitaonesha hali zao za biashara na uwekezaji, ikiwemo biashara za bidhaa na huduma, hali ya sekta za uzalishaji, uwekezaji, utalii na bidhaa maalumu. Lakini ni maonesho tu, hayatahusu biashara za papo hapo."

    Maonesho ya biashara za kampuni yatagawanyika katika sehemu za biashara za bidhaa na biashara za huduma. Kwenye maonesho hayo, kampuni kutoka nchi mbalimbali zitaonesha bidhaa zao, na kufanya biashara halisi. Bidhaa zitakazooneshwa kwenye maonesho hayo ni pamoja na vifaa vya hali ya juu vya simu za mkononi, vifaa vya kielektroniki na umeme vinavyotumiwa katika maisha ya watu, magari, nguo na mapambo, bidhaa za kawaida, mazao ya chakula, vifaa vya matibabu, dawa, teknolojia mpya, huduma za kuagiza, na uvumbuzi. Licha ya maonesho hayo mawili, shughuli nyingine za kuhimiza mawasiliano kati ya kampuni za kuuza na kununua zikiwemo kongamano la biashara za kimataifa la Hongqiao, semina na mikutano ya utoaji wa bidhaa mpya pia zitafanyika.

    Aidha, maonesho hayo pia yatazisaidia nchi zinazoendelea kuuza bidhaa zao nchini China. Naibu waziri wa biashara wa China Bw. Wang Bingnan amesema, China itapunguza au kusamehe gharama za kuhudhuria maonesho hayo. Anasema,

    "Sote tunajua kuwa China ina watu bilioni 1.3 na soko kubwa sana. Wachina wanahitaji bidhaa na huduma nzuri nyingi zaidi ili kuboresha maisha yao. Kupitia maonesho hayo, nchi zinazoendelea zitapata nafasi ya kuonesha bidhaa na huduma zao bora kwa wachina, na kunufaika kwa pamoja na soko kubwa la China. Nchi hizo pia zitasaidiwa kuongeza ushirikiano na China na nchi nyingine duniani, ili kutimiza mafanikio na maendeleo ya pamoja."

    Habari zinasema wizara ya biashara ya China na serikali ya Shanghai zimekamlisha mpango wa maonesho hayo, na kuanzisha ofisi ya utendaji kwa kuiga mfano wa maonesho ya biashara ya Guangzhou. Hadi sasa China imetoa mwaliko kwa wenzi wake zaidi ya 200 wa biashara, na inatarajia kampuni kutoka nchi zaidi ya 100 zitahudhuria maonesho hayo. Bw. Fu anasema,

    "Hatua ijayo ni kwamba tutafanya maandalizi mbalimbali kwa nguvu zote, na kuharakisha kusukuma mbele kazi za kuzialika kampuni zaidi, kuandaa semina, kufanya matangazo, na kukamilisha hatua za kuunga mkono, ili kuhakikisha maonesho hayo yanafanyika kwa mafanikio."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako