• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Watu watatu wauawa kwenye shambulio la kufyatua risasi Colorado Marekani

    (GMT+08:00) 2017-11-02 18:33:24

    Watu watatu wamefyatuliwa risasi na kuuawa jana jioni ndani ya supermarket ya Walmart huko Thornton, jimbo la Colorado nchini Marekani. Mshukiwa bado hajapatikana.

    Idara ya polisi ya Thornton awali ilitangaza kuwa watu wengi waliuawa kwenye shambulizi hilo lakini saa moja baadaye ikathibitisha kuwa wanaume wawili na mwanamke mmoja ndio waliouawa. Kwa mujibu wa ofisa wa Usalama wa Taifa, hadi sasa bado hawajua kama tukio hili linahusiana na ugaidi. Mbali na hayo polisi wamesema hawajui muuaji alikuwa na sababu gani.

    Mshukiwa huyo aliingia dukani na kuanza kufyatua risasi bila mpangilio ambapo wahanga hao watatu wote walikuwa kwenye eneo moja karibu na mbele ya duka, na baada ya shambulio hilo mshukiwa alikimbia kwenye eneo la tukio akiwa na gari aina ya ya Mitsubishi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako