• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Jamii ya Wachina nchini Zambia yaadhimisha miaka 53 ya uhusiano wa kibalozi kati ya nchi mbili

    (GMT+08:00) 2017-11-02 18:33:53

    Jamii ya Wachina nchini Zambia jana ilifanya onesho la kiutamaduni ili kusherehekea miaka 53 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kibalozi kati ya nchi hizo mbili.

    Tukio hilo, liliandaliwa na ubaloizi wa China wakishikiriana na Chama cha Wachina, na kushirikisha maonesho mengi ikiweno densi, muziki, maigizo na Kungfu katika eneo lililojengwa na serikali ya China. Waziri wa Utalii na Sanaa wa Zambia Charles Banda amesema anatarajia zaidi kubadilishana programu za utamaduni kati ya nchi mbili ili kupeana mawazo na uzoefu kwenye maendeleo ya ubunifu wa sanaa na sekta ya utamaduni. Pia ameipongeza China kwa kuendelea kusaidia maendeleo ya Zambia, akisema serikali inaendelea kutimiza wajibu wake chini ya makubaliano mbalimbali yaliyosainiwa kati ya pande mbili.

    Naye Balozi wa China nchini Zambia Yang Youming amesema kuendeleza urafiki wa kiutamaduni kati ya China na Zambia kutaleta maelewano ya pande mbili, mafungamano ya karibu na kupanua ushirikiano.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako