• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Bw. Guterres ataka ujenzi wa mtandao wa nishati duniani uzingatie uvumilivu na uendelevu

    (GMT+08:00) 2017-11-02 19:12:41

    Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres amesema, ujenzi wa mtandao wa nishati duniani unatakiwa kuzingatia uvumilivu na uendelevu.

    Bw. Guterres amesema hayo huko New York alipohudhuria kongamano lenye kaulimbiu ya "Mtandao wa Nishati Duniani: Kuhimiza Kutimiza Malengo ya Maendeleo Endelevu" ulioandaliwa na idara ya mambo ya kiuchumi na kijamii ya Umoja wa Mataifa na Shirika la ushirkiano na maendeleo ya mtandao wa nishati duniani.

    Kongamano hilo lililoshirikisha wataalamu na wasomi zaidi ya mia tatu limetoa Mpango wa Operesheni ya Ajenda za Maendeleo Endelevu mwaka 2030 za Umoja wa Mataifa wa Mtandao wa Nishati Duniani. Mpango huo umebuni njia halisi ya kujenga mtandao huo, huku ukidhihirisha operesheni katika pande 10 zikiwemo usambazaji wa mawazo, maendeleo ya nishati safi, kuunganisha mitandao ya umeme, mtandao wa umeme wa kisasa, kuinua ufanisi, kuhimiza uvumbuzi, ujenzi wa uwezo na sera za kuhakikisha.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako