• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yasema kutatua suala la nyuklia la Peninsula ya Korea kwa njia ya kidiplomasia kunaligana na maslahi ya pamoja ya pande husika

    (GMT+08:00) 2017-11-02 19:13:46

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bibi Hua Chunying amesema, kutatua suala la nyuklia la Peninsula ya Korea kwa njia ya kidiplomasia kunalingana na maslahi makubwa ya pamoja ya pande husika, ambayo pia ni matarajio ya jumuiya ya kimataifa.

    Bibi Hua Chunying ametoa kauli hiyo baada ya rais Moon Jae-in wa Korea Kusini kutoa hotuba kwenye kikao cha bunge akisema, lengo kuu la nchi hiyo ni kutimiza amani ya peninsula hiyo, na katika hali yoyote mapigano hayatatokea.

    Bibi Hua amesisitiza kuwa, China na Korea Kusini zina makubaliano muhimu na maslahi ya pamoja katika kulinda amani na utulivu wa peninsula ya Korea na kutatua kwa amani suala la nyuklia la peninsula hiyo. Aidha amesema China inaunga mkono pande husika kufanya juhudi zaidi za mawasiliano na mazungumzo, na kupenda kuimarisha mawasiliano na uratibu na upande wa Korea Kusini ili kuhimiza suala hilo lirudi katika meza ya mazungumzo haraka iwezekanavyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako