• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya:Mgomo wa wafanyikazi wa mashamba ya majani chai kuendelea

    (GMT+08:00) 2017-11-02 20:29:31

    Katibu mkuu wa Muungano wa vyama vya wafanyakazi nchini (COTU) Francis Atwoli amesema mgomo wa wafanyakazi wa mashamba ya majani chai ni wa kushutumu vitisho vya waajiri kwa wafanyakazi kwa kutumia polisi.

    Akiwahutubia waandishi wa habari nyumbani kwake huko Kajiado Atwoli alisema mgomo huo ni wa kuwahimiza wafanyakazi waendelee na mgomo wao hadi pale makubaliano ya pamoja yatakapotekelezwa.

    Atwoli aliutaja mgomo huo kuwa halali na akawahimiza maafisa wa polisi kuwa mbali na wafanyakazi hao akidai kuwa kumekuwa na taarifa za kuhangaishwa na maafisa wa polisi.

    Alisema waajiri wanaendelea kuwanyanyasa wafanyakazi kupitia rufaa za mahakama ili kuchelewesha utekelezaji wa makubaliano ya pamoja yanyonuia kutimiza maslahi ya wafanyakazi.

    Atwoli pia aliwaonya wanasiasa dhidi ya kutumia mgomo huo kuelezea ajenda zao za kisiasa. Wafanyakazi wa mashamba majani chai katika maeneo ya Kericho, Nandi, Sotik na sehemu nyinginezo wamekuwa kwenye mgomo kwa muda wa wiki mbili zilizopita.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako