• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda:Uchumi wa Rwanda kupungua kwa asilimia 5.2

    (GMT+08:00) 2017-11-02 20:29:51

    Rwanda itakosa kufikia malengo ya ukuwaji wake wa uchumi mwaka huu kwa mujibu wa shirika la kimataifa la fedha.

    Kwa mujibu wa shirika hilo,uchumi wa Rwanda utakuwa kwa asilimia 5.2 kutoka kwa asilimia 6.2.

    Rwanda ililenga kupata mafanikio hayo kutoka kwa kilimo,mauzo ya bidhaa nje na biashara.

    Laura Redifer amesema ukame uliotatiza sekta ya kilimo mwaka huu umechangia kuvuruga ukuwaji wa uchumi Rwanda.

    Aidha miradi ya miundo msingi ya Rwanda ya mwaka jana haikufanikiwa kama ilivyopangwa na idara tofauti.

    Hata hivyo Rwanda imeandikisha ukuwaji bora wa uchumi ikilinganishwa na nchi nyingine na eneo la jangwa la sahara.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako