• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • UNHCR yalitaka baraza la usalama la umoja wa mataifa kushughulikia vyanzo vya tatizo la wakimbizi

    (GMT+08:00) 2017-11-03 08:19:14

    Mkuu wa Shirika la kuhudumia wakimbizi la umoja wa mataifa UNHCR Bw Fillipo Grandi, amelitaka baraza la usalama la umoja wa mataifa kushughulikia vyanzo vya migogoro inayosababisha tatizo la wakimbizi duniani.

    Akiongea kwenye baraza la usalama la umoja wa mataifa Bw. Grandi amefahamisha hali halisi inayoikabili jumuiya ya kimataifa kwa sasa, ya migogoro mikubwa inayofanya kuwe na wakimbizi karibu katika maeneo yote duniani. Amesema kwa sasa idadi ya watu waliolazimika kukimbia makazi yao duniani imefika milioni 66, ikiongezeka kutoka watu milioni 42 wa mwaka 2009, hawa ni pamoja na wakimbizi milioni 17.2 wanaohudumiwa na shirika la kuhudumia wakimbizi.

    Bw. Grandi ametaja migogoro ya Syria na Iraq kuwa ni chanzo kilichosababisha robo ya watu wote kukimbia makazi yao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako