• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Cote d'Ivoire yazindua mradi mkubwa wa kuzalisha umeme kwa maji uliojengwa na kampuni ya China

    (GMT+08:00) 2017-11-03 08:19:33

    Kituo kikubwa cha kuzalisha umeme kwa nishati ya maji cha Soubre kilichojengwa na kampuni ya China nchini Cote d'Ivoire, kikiwa na uwezo wa kuzalisha megawati 275 za umeme kimezinduliwa jana.

    Mradi huo uliopangwa kujengwa kwa miaka mingi iliyopita, haukujengwa kutokana na ukosefu wa fedha. Ujenzi wake ulianza mwaka 2013 kwa fedha kutoka China.

    Rais Alassane Ouattara amesema serikali ya Cote d'Ivoire imeridhika na ubora na kasi ya ujenzi wa mradi huo, na kusema nchi yake iko tayari kuendelea kushirikiana zaidi na China.

    Konsela wa ubalozi wa China nchini Cote d'Ivoire Bw. Wang Jun amesema bwawa hilo ni moja ya mafanikio makubwa ya ushirikiano kati ya China na Cote d'Ivoire, na limechangia kuhimiza ushirikiano wa kibiashara kati ya pande mbili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako