• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Promota Eddie Hearn amemtaka Tyson Fury kuachana mitandao ya kijamii na kujikita katika mazoezi

    (GMT+08:00) 2017-11-03 08:30:12

    Promota maarufu nchini Uingereza, Eddie Hearn amemtaka bondia, Tyson Fury kuachana na maswala ya mitandao ya kijamii na badala yake ajikite zaidi katika mazoezi kwakuwa pambano lake lijalo hapo mwakani dhidi ya Anthony Joshua litakuwa ni la kihistoria. Hearn ambaye anamkataba wa matangazo ya ngumi na Sky Sports huku akiwasimamia mabondia Anthony Joshua, Ryan Burnett, James DeGake na Khalid Yafai amemtaka bingwa huyo wa zamani Fury ambaye anakabiliwa na kesi ya matumizi ya dawa zilizokatazwa michezoni (UKAD) kuwa bize na mazoezi kwaajili ya pambano hilo huku akiahidi kumsaidia juu ya janga linalomkabili. Baada ya Anthony Joshua kutetea ubingwa wake wa WBA na IBF kwa ushindi wa "knockout" dhidi ya Carlos Takam promota huyo anaamini niwakati wa kupigana na Fury ilikuwapatia furaha mashabiki wa mchezo huo nchini Uingereza.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako