• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania yawahukumu adhabu ya kifo watu 34 kutokana na kuwaua albino

    (GMT+08:00) 2017-11-03 08:54:00

    Ofisi ya mwendesha mashtaka mkuu wa serikali ya Tanzania imesema watu 34 wamekutwa na hatia ya kuwaua watu wenye ulemavu wa ngozi Albino, na walihukumiwa kifo kwa kunyongwa kati ya mwaka 2006 hadi 2016.

    Mwanasheria wa idara ya mwendesha mashtaka Bibi Beatrice Mpembo amesema hayo kwenye mkutano ulioandaliwa na Tume ya Taifa ya Haki za Binadamu na Utawala Bora CHRAGG mjini Dodoma, akiongeza kuwa kesi 67 za mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi bado zinasubiri hukumu.

    Amesema kuna haja ya kuwafahamisha wananchi kuhusu mauaji ya albino kwa sababu polisi hawawezi kupunguza tatizo hilo peke yao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako