• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mtuhumiwa wa shambulizi kwenye Supamaketi ya Walmart Marekani akamatwa

    (GMT+08:00) 2017-11-03 08:54:41

    Polisi nchini Marekani wamethibitisha kukamatwa kwa mtuhumiwa wa mauaji ya watu watatu kwenye supamaketi ya Walmart katika jimbo la Colorado nchini humo.

    Mtuhumiwa huyo mwenye umri wa miaka 47 alitajwa na mashahidi kama ni muuaji katili. Polisi wamesema mtuhumiwa huyo aliingia kwenye duka hilo kutoka lango la kusini na kuanza kufyatua risasi ovyo, kisha akakimbia kutoka eneo la tukio kwa kutumia gari nyekundu.

    Polisi pia wamefafanua kuwa madhumuni ya mtuhumiwa huyo bado haijajulikana, lakini hakuna dalili kwamba tukio hilo linahusiana na ugaidi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako