• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri mkuu wa Uingereza amteua waziri mpya wa ulinzi

    (GMT+08:00) 2017-11-03 09:02:01

    Waziri mkuu wa Uingereza Bibi Theresa May amemteua kiongozi wa chama cha wahafidhina bungeni Bw Gavin Williamson kuwa waziri wa ulinzi, kuchukua nafasi ya Bw Michael Fallon aliyejiuzulu ghafla.

    Bw. Williamson ambaye hajawahi kuingia kwenye baraza la mawaziri na hana uzoefu wa mambo ya kijeshi, atakabiliwa na changamoto tatu za kuzuia kupunguzwa kwa bajeti ya ulinzi, kuongeza mishahara ya wanajeshi na kupambana na makundi ya kigaidi kama vile kundi la IS.

    Bw. Williamson alizaliwa mwaka 1976, na mwaka 2001 alichaguliwa kuwa mbunge wa jimbo la Stafford kusini. Mwaka 2010 aliingia kwenye baraza la makabwela la bungle la Uingereza na kuwa msaidizi wa aliyekuwa waziri mkuu Bw David Cameron katika bunge hilo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako