• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sudan Kusini yakanusha shutuma za kuunga mkono makundi ya upinzani ya Sudan

    (GMT+08:00) 2017-11-03 09:02:19

    Rais Salva Kiir Mayardit amekanusha shutuma kuwa nchi yake inayaunga mkono makundi ya upinzani ya Sudan.

    Akikutana na wanahabari pamoja na mwenzake wa Sudan Omar al-Bashir, Bw. Kiir amesema shutuma hizo hazina msingi, na Sudan Kusini haina sababu yoyote ya kuyaunga mkono makundi yenye silaha ya Sudan.

    Bw. Al-Bashir amesisitiza msimamo wa Sudan wa kutounga mkono kundi lolote lenye silaha la Sudan Kusini, na kusema kuyaunga mkono makundi ya upinzani kutaathiri utulivu wa eneo la mpaka kati yao. Pia ameeleza matarajio ya kujenga uhusiano wa kawaida na Sudan Kusini.

    Bw. Kiir aliwasili jana mjini Khartoum kwa ziara ya siku mbili, ambako atafanya mazungumzo na serikali ya Sudan kuhusu masuala ya usalama hasa utekelezaji wa makubaliano ya ushirikiano.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako