• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Cavani asema si lazima yeye na Neymar wawe marafiki

  (GMT+08:00) 2017-11-03 09:35:24

  Straika wa PSG ya Ufaransa, Edinson Cavani amefunguka kuwa suala la penati kwake limeshapita lakini hadhani kwamba ni lazima yeye na straika mwenzake Neymar wawe marafiki. Akiongea kwenye mahojiano maalum, Cavani amesema anachohitaji yeye ni kushirikiana tu uwanjani ili timu ifanye vizuri. Akizungumzia tetesi za yeye kupokonywa jukumu la kupiga penati, Cavani alisema hilo ni suala la kocha, yeye ndiye atakayetoa majibu ya jambo hilo baada ya kufanya maamuzi. Neymar na Cavani walitofautiana katika mchezo wa ligi kuu nchini Ufaransa dhidi ya Lyon baada wawili hao kugombea kupiga penati kabla Cavani hajachukua mpira na kukosa penati hiyo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako