• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sudan yakanusha kuunga mkono jeshi la upinzani nchini Sudan Kusini

    (GMT+08:00) 2017-11-03 18:37:51

    Rais Omar al-Bashir wa Sudan amekanusha lawama kutoka kwa mwenzake wa Sudan Kusini Salva Kiir ambaye yuko zarani nchini Sudan, kuwa nchi hiyo inaunga mkono makundi ya upinzani nchini Sudan Kusini, akisema anapenda kujenga uhusiano wa kawaida wa pande mbili na Sudan Kusini.

    Rais Kiir ameilaumu serikali ya Sudan kuwa inatoa uungaji mkono kwa makundi ya upinzani nchini Sudan Kusini, kwa kuyapatia silaha makundi hayo. Pia amekanusha kuwa Sudan Kusini inayaunga mkono makundi ya upinzani ya Sudan.

    Rais al-Bashir amesisitiza kuwa Sudan haitaunga mkono kundi lolote la upinzani nchini Sudan Kusini, na inapenda kujenga uhusiano wa kawaida wa pande mbili na nchi hiyo.

    Rais Kiir aliwasili huko Khartoum juzikwa kufanya ziara ya siku mbili nchini humo. Pande mbili zitafanya mazungumzo yanayofuatilia suala la usalama, hasa hali ya utekelezaji wa makubaliano ya ushirikiano yaliyosainiwa na nchi hizo mbili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako