• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yaandaa muswada wa kanuni ya uwekezaji nje ya nchi

    (GMT+08:00) 2017-11-03 18:57:03

    Idara ya taifa ya maendeleo na mageuzi ya China imetoa rasimu ya kanuni ya kurahisisha taratibu za kiutawala kuhusu uwekezaji na kuimarisha kanuni za uwekezaji nje ya nchi.

    Kanuni mpya inaondoka kipengele kilichowekwa mwaka 2014 kinachotaka makampuni yanayotaka kuchukua au kuomba zabuni kwenye miradi ya nje, iwe na mtaji usiopungua dola za kimarekani milioni 300. Mbali na kuondoa kanuni hiyo, rasimu hiyo pia inarahisisha utaratibu wa ruhusa na kulegeza mahitaji ya muda wa ukomo kwa makampuni kupata ruhusa.

    Katika miaka ya hivi karibuni uwekezaji wa moja kwa moja wa nje kutoka China umekuwa ukiongezeka kwa kasi, lakini kuanzia mwaka jana serikali ya China imeweka utaratibu mkali wa kuondoka desturi zisizo nzuri kwenye eneo hilo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako