• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wanajeshi wa Kenya wawaua wapiganaji wawili wa kundi la Al Shabaab

    (GMT+08:00) 2017-11-03 19:30:40

    Jeshi la Kenya limesema limewaua wapiganaji wawili wa kundi la Al Shabaab wakati ikivunja shambulizi la kundi hilo kwenye kaunti ya Lamu.

    Msemaji wa jeshi la Kenya Davd Obonyp amesema wanajeshi hao pia wameongeza msako wa wapiganaji waliojeruhiwa.

    Habari zinasema wanajeshi wa Kenya waliokuwa kwenye doria katika eneo la Witu walipambana vikali na wapiganaji wawili wa kundi hilo. Bw. Obonyo amesema bado wanaendelea kuwasaka wapiganaji waliojeruhiwa na kukimbilia katika msitu wa boni, na idadi ya vifo inaweza kuongezeka.

    Tukio hili limetokea siku chache baada ya jeshi la Kenya kuwaua wapiganaji wanne wa kundi la Al Shabaab, na kukamata silaha zao katika eneo la Mararani, Lamu mashariki.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako