• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sekta ya utalii yapata pigo

    (GMT+08:00) 2017-11-03 20:44:42

    Sekta ya utalii nchini Kenya imepata pigo kubwa baada ya meli ya kifahari ya MS Albatros kukatiza safari ya kwenda mjini Mombasa. Afisa wa uhusiano mwema wa halamshauri ya bandari Bw Haji Masemo amersema meli hiyo ilikatiza safari yake bila maelezo yoyote. Masemo ameongeza kuwa baada ya meli hiyo kukatiza safari yake hivi sasa hakuna meli nyingine ambazo zinatarajiwa kuwasili Mombasa katika msimu huu wa watalii. Katika msimu uliopita, ni meli mbili tu ambazo ziliwasili mara mbili na watalii wapatao 2,958. Mwaka wa 2015 meli kumi za kifahari ziliwasili na watalii 6000. Wakati huo huo mwenyekiti wa chama cha watoaji huduma za hoteli tawi la Pwani Bw Sam Ikwaye amesema watalii wanaozuru Kenya kwa kupitia bandari huleta manufaa makubwa kwa mbuga za wanyama pori, wauzaji vinyago na biashara mbali mbali.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako