• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Vigogo wa kampuni ya madini ya ACACIA wajiuzulu

    (GMT+08:00) 2017-11-03 20:45:10

    Kampuni ya Acacia imebainisha kuwa ofisa Mtendaji Mkuu wake Brad Gordon na afisa Mkuu wa Fedha Bw. Andrew Wray wamejiuzulu.

    Acacia ni moja ya kampuni kubwa za uchimbaji wa madini ya dhahabu Afrika na ina migodi mitatu Kaskazini- Magharibi mwa Tanzania, ambazo ni Bulyanhulu mkoani Shinyanga, Buzwagi wilayani Kahama mkoani Shinyanga na North Mara wilayani Tarime mkoani Mara. Kampuni hiyo imetangaza kuwa wawili hao wataondoka rasmi Acacia mwishoni mwa mwaka huu.

    Kujiuzulu kwa viongozi hao wawili, kumekuja takribani miezi miwili tangu kampuni hiyo ya Acacia kumaliza mgogoro wake na Serikali ya Tanzania kuhusu udanganyifu katika usafirishwaji wa mchanga wa madini nje ya nchi. Mgogoro huo ulianza baada ya Rais John

    Magufuli kupiga marufuku kusafirishwa nje ya nchi kwa mchanga wa madini wa Kampuni ya Barrick kwa kile ambacho ilisema ni kuwepo kwa udanganyifu kuhusu thamani ya madini yaliyomo kwenye mchanga huo. Hata hivyo, viongozi hao wawili waliojiuluzu pamoja na timu ya viongozi na watalaamu mbalimbali kutoka Tanzania walifikia makubaliano ya kumaliza mgogoro huo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako