• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kampuni ya Nakumatt yaendelea kufunga matawi yake

    (GMT+08:00) 2017-11-03 20:45:28

    Duka la jumla la Nakumatt limefunga tawi la Kisii na kuzidisha masaibu yanayokumba duka hilo ambalo ni mojawapo ya maduka makubwa zaidi nchini Kenya. Taarifa hii inakuja wakati ambapo kwa kipindi cha miezi kumi wateja wamekuwa wakilalamikia huduma mbaya baada ya kukosa kupata bidhaa muhimu katika duka hilo. Kwingineko ni kuwa ukarabati wa barabara ya mradi wa Northern Corridor B unatarajiwa kupunguza msongamano wa magari katika kaunti ya Busia.Mamlaka ya barabara kuu nchini Kenya KENHA imesema mbali na kukarabati sehemu ya barabara hiyo karibu na kituo cha mabasi mjini Busia pia itapanua barabara hiyo kutoka eneo la Korinda.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako