• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • ZAECA kuwachukulia hatua maofisa 9 kwa tuhuma za kuhusika na ufisadio

    (GMT+08:00) 2017-11-03 20:45:54

    Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa kisiwani Zanzibar (ZAECA), imesema wizara tisa za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) pamoja na watendaji wake wamebainika kufanya vitendo vya ubadhirifu wa fedha za umma.

    Kwa mujibu wa afisa wa uchunguzi katika taasisi hiyo Bw Khamis Bakari, shilingi bilioni 1.6 zimebainika kupotea katika wizara hizo pamoja na taasisi za vikosi vya ulinzi vya Zanzibar.Bakari ameongeza kuwa kazi inayofanywa kwa sasa ni kukamilisha uchunguzi na kuwasilisha ripoti kamili kwa mkurugenzi wa mashtaka na Makosa ya Jinai Zanzibar (DPP). Miongoni mwa wizara ambazo zilihusika ni pamoja na Wizara ya Fedha na Mipango, Wizara ya Afya, Wizara ya Biashara, Viwanda na Masoko pamoja na Wizara ya Habari, Utangazaji, Utalii na Michezo.

    Mwishoni mwa wiki, Waziri wa Fedha na Mipango Bw Khalid Salum Mohamed alikiri kuwepo kwa ubadhirifu mkubwa wa fedha huku watendaji 21 wakihusishwa na shutuma hizo. Alisema madai yote ya ubadhirifu wa mali ya umma kwa watumishi wa serikali yamepelekwa kwa mamlaka ya rushwa na sasa yapo katika hatua za mwisho kufikishwa Mahakamani kwa ajili ya kufunguliwa kesi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako