• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Maonyesho ya kuadhimisha miaka 40 ya uwepo wa reli ya TAZARA yafanyika Zambia

    (GMT+08:00) 2017-11-04 18:44:12

     

    Serikali za China na Zambia zimefanya maonyesho ya kuadhimisha miaka 40 ya kuanzishwa kwa reli ya TAZARA mjini Lusaka, ambayo uzinduzi wake umeshuhudiwa na rais Kenneth Kaunda wa Zambia na balozi wa China nchini humo Yang Youming.

    Waziri ofisi ya makamu wa rais Bi. Sylvia Chalikosa amesema kwenye uzinduzi wa maonyesho hayo kuwa lengo la maonyesho hayo ni kuonyesha hatua za ujenzi wa reli hiyo na umuhimu wake kwa nchi isiyo na bandari kama Zambia. Amewasifu wachina na wazambia waliojitolea maisha yao wakati wa ujenzi wa reli hiyo na kuishikuru China kujitolea kusaidia mradi huo hata pale ambapo China ilipitia mtikisiko wa kiuchumi.

    Naye Balozi wa China nchini Zambia Bwana Yang Youming amesema mradi huo wa kirafiki ulianzishwa na viongozi wa nchi hizo tatu na kuwa reli hii imechukua nafasi muhimu kwa maendeleo ya uchumi si tu kwa Zambia na Tanzania pia na nchi nyingine jirani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako