• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Polisi wa Zimbabwe wakamata raia wa Marekani kwa tuhuma za kumtusi Mugabe

    (GMT+08:00) 2017-11-04 18:45:05

    Polisi nchini Zimbabwe imemkamata raia mmoja wa Marekani na kuchukua kompyuta yake kutokana na tuhuma za kumtukana rais Robert Mugabe kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii.

    Bibi Martha O'Donovan raia wa Marekani anayefanya kazi katika televisheni ya Magamba alitiwa mbaroni asubuhi ya Ijumaa na wakili wake ObeyShava, ameviambia vyombo vya habari kuwa O'Donovan alikuwa ametuhumiwa kwa kusema "Tunaongozwa na mwanamume mnafiki na mwenye ugonjwa" katika ukarasa wake wa Twitter, ujumbe huo ambao pia una picha inayoonesha rais Mugabe mwenye umri wa miaka 93 akitumia mpira wa kumsaidia haja ndogo.

    Hata hivyo, Chama cha Mawakili wa Kutetea Haki za Binadamu nchini humo ZLHR kimesema ujumbe huo ulioandikwa katika mtandao wa Twitter haukutaja jina la rais Mugabe.

    O'Donovan ni mtu wa kwanza aliyekamatwa kuhusiana na twitter baada ya serikali ya Zimbabwe kuunda wizara ya usalama wa mtandao mwezi uliopita.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako