• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Uturuki aapa kuangamiza kambi za ugaidi nchini Iraq na Syria

    (GMT+08:00) 2017-11-04 19:10:25

    Rais Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki ameapa kuharibu kambi zote za ugaidi nchini Iraq na Syria.

    Alipotoa hotuba katika mkoa wa magharibi wa Manisa, rais Erdogan amesema nchi yake imeamua kulinda wananchi wake na kuwaangamiza magaidi nje ya Uturuki. Ameongeza kuwa mtu yeyote anayakaa pamoja na magaidi ndiye mgaidi, huku akilaani nchi washirika wa magharibi ikiwemo Marekani kwa kuunga mkono wanamgambo wa kundi la PKK na kundi la Kikurdi nchini Syria.

    Uturuki inaorodhesha kundi la PKK na kundi la wanamgambo la kikurdi la Syria linalojulikama kama People's Protection Unit kama makundi ya kigaidi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako