• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano na waandishi wa habari kuhusu rais wa Marekani kufanya ziara nchini China wafanyika

    (GMT+08:00) 2017-11-04 20:03:51

    Mkutano na waandishi wa habari kuhusu rais Donald Trump wa Marekani kufanya ziara nchini China umefanyika jana hapa Beijing, ambapo naibu waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Zheng Zeguang amejulisha kazi ya maandalizi kuhusu ziara hiyo.

    Bw. Zheng amesema vikundi vya kazi vya China na Marekani vimedumisha mawasiliano na ushirikiano wa karibu, na kazi ya maandalizi inaendelea vizuri. .

    Bw. Zheng amesema China na Marekani zina maslahi ya pamoja katika kudumisha amani na utulivu wa dunia, na kuhimiza maendeleo na ustawi duniani. China inapenda kushirikiana na Marekani kuhimiza mkutano kati ya marais Xi Jinping na Trump kupata mafanikio, ili kuwanufaisha zaidi wananchi wa nchi hizo mbili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako