• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ubalozi mdogo wa China uliopo Zanzibar watoa msaada kwa kituo cha watoto yatima

    (GMT+08:00) 2017-11-05 16:43:54

    Ubalozi mdogo wa China uliopo Zanzibar jana umefanya hafla ya kutoa msaada wa vitu kwa kituo cha watoto yatima. Watu zaidi ya 100 wakiwemo mke wa balozi mdogo wa China Bibi Liu Jie, mke wa rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, maofisa wa idara za serikali ya Zanzibar zinazoshughulikia mambo ya wanawake, afya na michezo, madaktari wa China wanaotoa msaada huko, walimu na wanafunzi wa Chuo cha Confucius, walimu na watoto wa kituo cha watoto yatima wamehudhuria hafla hiyo.

    Bibi Liu Jie amesema ubalozi mdogo umeandaa shughuli hiyo ili kuunga mkono kazi ya kuwahudumia watoto yatima kisiwani humo.

    Mama Mwanamwema Shein ametoa shukrani kwa ubalozi mdogo wa China na kusema shughuli hiyo si kama tu imewapatia watoto yatima vitu vya kuandikia, kuchezea watoto na vinavyotumiwa kila siku, bali pia imewapatia upendo na afya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako