• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Russia yatuma ndege za mabomu kushambulia majengo ya kundi la IS

    (GMT+08:00) 2017-11-05 16:44:18

    Wizara ya ulinzi ya Russia imetangaza kuwa jana jeshi la anga la Russia limetuma ndege za mabomu aina ya Tu-22M3 kushambulia majengo ya kundi la IS nchini Syria.

    Wizara hiyo inasema ndege hizi ziliruka nchini Russia, kupita anga ya Iraq na Iran, kushambulia majengo ya kundi la IS yaliyoko mjini Abu Kamel mashariki mwa Syria, na kubomoa ghala za silaha na makao makuu ya kundi hilo.

    Jeshi hilo na jeshi la maji la Russia lililokaa katika bahari ya Mediterranean yameunga mkono jeshi la serikali ya Syria kupambana na kundi la ISkwa siku tano mfululizo kuanzia tarehe 31 Oktoba.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako