• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Marais wa Tanzania na Uganda kuweka jiwe la msingi ujenzi wa bomba la mafuta.

    (GMT+08:00) 2017-11-05 18:22:47

    Rais wa Tanzania John Magufuli anatarajia kwenda nchini Uganda akiwa huko pamoja na mshirika wake Rais wa Uganda Yoweri Museveni wataweka jiwe la msingi kwa ujenzi wa bomba la mafuta ghafi.

    Kwa mujibu wa taarifa ya wizara ya mambo ya nje iliyotolewa jumapili, uwekaji huo wa jiwe la msingi utafanyika tarehe 11 mwezi huu mjini Hoima.

    Ujenzi wa bomba hilo ambalo litapitia baharini hadi mkoa wa Tanga nchini Tanzania utafanywa na kampuni ya Total ya Ufaransa, kampuni ya kitaifa ya mafuta ya baharini ya China CNOOC na Kampuni ya mafuta ya Tullow ya Uingereza na tayari makampuni haya ya mafuta yameanza utafutaji wa mafuta nchini Uganda.

    Kwa mujibu wa takwimu za serikali ya Uganda, ujenzi huo utagharimu dola za kimarekani bilioni 3.5 na unatarajiwa kukamilika mwaka 2020 ukiwa ni kilomita 1,445.

    Marais hao wawili waliweka jiwe la msingi kwa upande wa Tanzania mwezi Agusti mwaka huu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako