• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Misri yalaani kundi la Houthi kuishambulia Saudi Arabia kwa makombora

    (GMT+08:00) 2017-11-06 08:25:55

    Misri imelaani vikali kundi la waasi la Houthi la madhehebu ya Shia nchini Yemen kuishambulia Saudi Arabia kwa makombora.

    Taarifa iliyotolewa na wizara ya mambo ya nje ya Misri imesema, serikali ya Misri na watu wake wanaiunga mkono serikali ya Saudi Arabia na watu wake na kuunga mkono Saudi Arabia kuchukua hatua za kujilinda usalama na utulivu dhidi ya shambulizi la kikatili.

    Kwa mujibu wa shirika la habari la Saba linalodhibitiwa na kundi la Houthi, kundi hilo lilirusha makombora dhidi ya uwanja wa ndege wa kimataifa wa King Khalid mjini Riyadh jumamosi usiku. Serikali ya Saudi Arabia ilisema makombora yalianguka na kulipuka kaskazini mwa uwanja huo bila kusababisha hasara yoyote.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako