• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uchaguzi wa rais wa DRC wapangwa kufanyika Desemba wa mwaka 2018

    (GMT+08:00) 2017-11-06 08:46:09

    Tume ya uchaguzi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (CENI) imetangaza kuwa uchaguzi mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) utafanyika tarehe 23, mwezi wa Desemba mwaka kesho.

    Mwenyekiti wa CENI Bw Corneille Nangaa amesema, uchaguzi wa wabunge na wa majimboni pia utafanyika pamoja na uchaguzi wa rais ili kupunguza gharama za uchaguzi.

    Habari zinasema rais mpya atakayechaguliwa ataapishwa tarehe 13, mwezi wa Januari, mwaka 2019.

    Wapinzani ambao wamekuwa wanamshutumu Rais Joseph Kabila kwa kuwa chanzo cha mkwamo wa kisiasa nchini humo, wamepinga ratiba hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako