• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Majadiliano kuhusu Syria yaahirishwa

    (GMT+08:00) 2017-11-06 09:15:49

    Russia imesitisha majadala wa makubaliano kuhusu Syria kufuatia mvutano uliojitokeza kuhusu ushiriki wa Chama cha Kikurd cha nchini Syria.

    Ikulu ya Uturuki imeendelea kupingana na uamuzi huo, ambao imeutaja kuwa unazorotesha jitihada za kutafuta suluhu ya kudumu nchini Syria.

    Kabla ya tangazo la kusitisha mazungumzo, Russia iliarifu juu ya uwepo wa majadiliano juu ya Syria mnamo Novemba 18 mjini Sochi ambayo yangejumuisha vikundi 33 vya Syria, vyama vya kisiasa pamoja na makundi ya Kikurd na baadhi ya vikundi vya waasi vinavyoipinga serikali ya Rais Assad.

    Wakati huo huo, watu 75 wameuawa na wengine 140 arobaini wamejeruhiwa kufuatia mlipuko wa bomu lililokuwa limetegwa kwenye gari katika mji Deir al Zour mashariki mwa Syria. Taarifa inaeleza kuwa kundi la Islamic State (IS) linadhaniwa kuhusika na tukio hilo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako