• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Idadi ya watu wanaounga mkono Finland kujiunga na NATO yapungua

    (GMT+08:00) 2017-11-06 09:26:45

    Kura za maoni nchini Finland zinaonyesha kuwa asilimia 59 ya watu wa Finland wanapinga kujiunga na NATO. Uchunguzi uliofanywa na gazeti la Helsingin Sanomat (HS), unaonyesha kuwa asilimia 22 ya watu waliohojiwa wanaunga mkono Finland kujiunga na NATO, asilimia 19 hawajui.

    Matokeo ya sasa ni tofauti na ya mwaka 2014 ambayo yalionyesha kuwa asilimia 57 ya watu walipinga kujiunga na NATO na asilimia 26 waliunga mkono.

    Matokeo hayo yametolewa wakati waziri wa Ulinzi wa Marekani Bw James Mattis anafanya ziara nchini Finland na anatarajiwa kufanya mazungumzo na Rais wa nchi hiyo na waziri wa Ulinzi. Wanasiasa waandamizi wa Finland wanaona kuwa ushirikiano wa kijeshi kati ya Finland na Marekani umepiga hatua.

    Nchini Finland Bw. Mattis na mwenzake wa Finland watasaini makubaliano kuhusu kubadilishana data za usimamizi wa anga.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako