• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Iran yasema kujiuzulu kwa waziri mkuu wa Lebanon kutasababisha hali ya wasiwasi ya kikanda

    (GMT+08:00) 2017-11-06 10:46:52

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Iran Bw. Bahram Qasemi ametoa taarifa akisema, lengo la kujiuzulu kwa waziri mkuu wa Lebanon Bw. Saad Hariri ni kusababisha hali ya wasiwasi nchini Lebanon na sehemu ya Mashariki ya Kati.

    Bw. Qasemi amesema ni jambo la kushangaza na kusikitisha kwa waziri mkuu wa Lebanon kutangaza kujiuzulu katika nchi nyingine, hii inaonyesha kuwa, Bw. Hariri amekwenda mbali kwenye njia ya kusababisha hali ya wasiwasi ya kikanda.

    Bw. Hariri alitangaza kujiuzulu tarehe 4 wakati alipofanya ziara nchini Saudi Arabia. Alitoa hotuba kwa njia ya televisheni kuilaani Iran kuingilia kati mambo ya kanda hiyo na mambo ya nchi za kiarabu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako