• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Saudi Arabia yatangaza donge nono kwa watakaosaidia kukamatwa kwa viongozi wa kundi la Houthi la Yemen

    (GMT+08:00) 2017-11-06 17:53:09

    Saudi Arabia imetangaza kutoa donge nono la dola milioni mia 4.4 za kimarekani kwa watu watakaosaidia kukamatwa kwa viongozi 40 wa kundi la Houthi la Yemen.

    Serikali ya Saudi Arabia imetoa taarifa ikisema, viongozi 40 wa kundi la Houthi wamewekwa kwenye orodha ya watu wanaotafutwa na nchi hiyo kutokana na kushiriki shughuli za kigaidi. Nchi hiyo imeahidi kutoa donge nono la dola milioni 5 hadi 30 za kimarekani kwa watu wanaoweza kutoa taarifa zitakazosaidia kukamatwa kwa viongozi hao.

    Siku moja kabla ya Saudi Arabia kutoa ahadi hiyo, kundi la Houthi lilirusha kombora kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa huko Riyadh, lakini kikosi cha ulinzi wa anga cha nchi hiyo kilizuia na kuharibu kombora hilo. Hii ni mara ya kwanza kwa kundi hilo kurusha kombora kwenye mji mkuu wa Saudi Arabia.

    Habari nyingine zinasema, wizara ya mambo ya nje ya Qatar imetoa taarifa ikilaani shambulizi hilo dhidi ya Saudi Arabia. Taarifa hiyo imesema, shambulizi lolote la moja kwa moja au lisilo na lengo maalum dhidi ya raia wa kawaida ni kitendo kinachokiuka sheria ya kimataifa, ambacho kinapingwa vikali na Qatar.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako