• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mwenyekiti wa zamani wa jimbo la Catalonia azuiliwa kuondoka Ubelgiji

    (GMT+08:00) 2017-11-06 18:33:57

    Idara ya uendeshaji mashtaka ya Brussels, Ubelgiji imetangaza kumzuia mwenyekiti wa zamani wa jimbo lililojitangazia uhuru la Catalonia nchini Hispania, Bw. Carles Puigdemeont ambaye jana alijisalmisha kwa polisi, kuondoka Ubelgiji.

    Kwa mujibu wa sheria ya Ubelgiji, kesi hiyo itapelekwa na kujadiliwa katika mahakama, na uamuzi utatolewa ndani ya siku 15. Naibu waziri mkuu wa Ubelgiji, ambaye pia ni waziri wa mambo ya ndani Bw. Jan Jambon, amewaambia waandishi wa habari kwamba anatarajia Umoja wa Ulaya utaweka wazi msimamo wake juu ya suala hilo haraka iwezekanavyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako