• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yaunga mkono kifedha makampuni madogo

    (GMT+08:00) 2017-11-06 19:27:09

    China imetangaza sera za kodi zinazolenga kupunguza mzigo wa makampuni madogo na kuunga mkono ukuaji wa uchumi.

    Kwa mujibu wa waraka uliotolewa kwa pamoja na Wizara ya fedha na Idara ya kodi ya Taifa, kuanzia Disemba mosi, 2017 hadi Disemba 31 2019, taasisi za fedha zitasamehewa kodi ya ongezeko la thamani VAT kwenye mapato yao yanayotokana na riba za mikopo inayotoa kwa makampuni madogo na yanayomilikwa na mtu mmoja mmoja. Kwa sasa sera hiyo zinatumika kwa utoaji mikopo kwa wakulima tu.

    Wakati huohuo kodi za stempu kwenye mikataba ya mkopo kwa makampuni madogo pia zitaondolewa kuanzia Januari mosi, 2018 hadi Disemba 31, 2020.

    Serikali imekuwa ikihamasisha mabenki kuunga mkono makampuni madogo, ambayo mara nyingi yana ugumu wa kupata mikopo ya benki.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako