• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • WHO lapata ruzuku ya dola milioni 2 kusaidia mambo ya afya nchini Somalia

    (GMT+08:00) 2017-11-06 19:28:37

    Shirika la Afya Duniani WHO limesema limepokea ruzuku ya dola za kimarekani milioni 2 kusaidia ufuatiliaji wa magonjwa ya mlipuko na shughuli za mwitikio wa huduma za dharura za msingi za afya nchini Somalia.

    Mwakilishi wa WHO nchini Somalia Ghulam Popal amesema hatari ni kubwa miongoni mwa watu waliokimbia makazi na wale walio hatarini tayari wameshadhoofishwa na umasikini na lishe duni. Amesema ukosefu wa rasilimali za kutosha, wanandoa wasiopata huduma za afya na kutogunduliwa kwa wakati na kutokuwepo kwa muitikio wa milipuko ya magonjwa vimetoa changamoto katika juhudi za kuokoa maisha ya watu na kuzuia milipuko ya magonjwa nchini humo.

    Milipuko ya magonjwa ya kuambukiza bado ni tishio kubwa la afya ya umma nchini Somalia. Karibu watu milioni 5.5 wapo hatarini kupata kipindupindu, ambapo zaidi ya nusu ni wanawake na watoto chini ya umri wa miaka mitano.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako