• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya: Duka la Tuskys limeanza kurejesha bidhaa katika duka la Nakumatt

    (GMT+08:00) 2017-11-06 20:20:35

    Duka la Tusky limethibitisha mipango ya kusaidia kufufua duka la Nakumatt kupitia mkakati wa kurejesha bidhaa katika duka hilo.

    Programu hii ya kipekee ina lengo la kutoa jukwaa la msaada kwa Duka la Nakumatt kabla ya kushirikiana kibiashara;

    Mtendaji mkuu wa Tusker Mattresses Dan Githua, amesema mpango wa kurejesha bidhaa katika duka la Nakumatt unatarjiwa kuanza hivi karibuni, pia ameeleza mpango huu ni kama zoezi la kufufua biashara.

    Mpango wa kurejesha bidhaa katika duka la Nakummat amesema, unafanywa kwa kushirikiana na wauzaji wakuu wa rejareja kama sehemu ya kujitolea kwa pamoja kuunga mkono kufufuka kwa Nakumatt.

    Kwa mujibu wa Githua, awamu ya kwanza itahusisha urejeshaji upya wa bidhaa katika matawi saba muhimu Nairobi na Mombasa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako