• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sudan: bei za bidhaa zimepanda juu tena nchini sudan

    (GMT+08:00) 2017-11-06 20:21:45

    Watu nchini Sudan wanalalamika juu ya kuongezeka upya kwa bei ya chakula na bidhaa za wanunuzi.

    Wafanyabiashara huko Darfur walihusisha kuongezeka kwa bei na kodi nyingi wanazo lipa wafanyibiashara na ada zilizowekwa hivi karibuni kwenye bidhaa.

    Mfanyibiashara mmoja kutoka Darfur amezungumza na Radio Dabanga, na kusema ada za ziada zimeongezwa na mamlaka juu kwa bidhaa 400 zinazoja kutoka Khartoum.

    Hii imefanywa kwa sababu ya kulinda mikutano ya biashara kati ya mji mkuu na magharibi.

    Shirika la Kati la Takwimu la Sudan liliripoti mapema mwezi Oktoba kuwa mfumuko wa bei uliongezeka hadi asilimia 35.13 mwezi Septemba kutoka 34,61 mwezi Agosti.

    Mnamo Oktoba 31, Rais Omar Al Bashir aliamuru Wizara ya Fedha na Benki Kuu ya Sudan kuingilia kati na kudhibiti viwango vya ubadilishaji na kupunguza viwango vya mfumuko wa bei.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako