• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mazungumzo kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa yafunguliwa mjini Bonn kwa mwito wa kudumisha makubaliano ya Paris

    (GMT+08:00) 2017-11-07 09:18:14

    Mkutano wa 23 wa nchi zilizosaini makubaliano ya umoja wa mataifa kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa, umeanza jana mjini Bonn, Ujerumani kwa mwito wa kuendelea kufuata makubaliano ya Paris kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa.

    Mkutano huo una lengo la kuandaa mpango wa utekelezaji kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa, kwa lengo kupunguza utoaji wa hewa zinazosababisha kuongezeka kwa joto na kuweka malengo ya kuhakikisha ongezeko la joto duniani halifikii nyuzi mbili.

    Katibu mkuu anayeshughulikia kazi ya kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa Bibo Patricia Espisona ametaka hatua zichukuliwe kuhakikisha kuna mfumo kamili wa kutekeleza makubaliano hayo hatua kwa hatua.

    Mwakilishi wa China kwenye mkutano huo Bw. Xie Zhenhua, amesema kabla ya ufunguzi wa mkutano huo, kuwa China inatumai kuwa washiriki wataandaa rasimu inayozingatia mahitaji ya kila upande.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako