• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Baraza la Usalama lafikiria kuipa tena mamlaka Tume ya Kulinda amani nchini CAR

    (GMT+08:00) 2017-11-07 09:29:00

    Baraza la Usalama linafikiria kuipa tena mamlaka Tume ya Kulinda amani ya Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati MINUSCA, baada ya hali ya usalama kuwa tete nchini humo.

    Akiongea na wanahabari Mwenyekiti wa baraza hilo Bw. Sebastiano Cardi amesema hali nchini humo kisiasa, kijeshi na kibinadamu bado ni tete , hivyo baraza litajadili kwa kina kuhusu azimio la kuipa tena mamlaka tume hiyo katika siku chache zijazo. Hata hivyo hakutaka kusema kama baraza litapitisha pendekezo la katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres la kuongeza askari 900 kwenye tume hiyo. Mamlaka ya MINUSCA inamalizika Novemba 15.

    Mkuu wa tume ya MINUSCA Bw. Parfait Onanga-Anyanga ameliambia baraza la usalama kuwa pendekezo la Bw. Guterres la kuongeza askari 900 ni sehemu ya mkakati wa kina wa kukabiliana na hali inayozidi kuwa mbaya, na kutoa nafasi ya kuboresha mchakato wa kisiasa nchini humo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako