• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Israel yakamilisha kujenga ukuta wa mpakani

    (GMT+08:00) 2017-11-07 10:20:28

    Israel imetekeleza mpango wa kujenga ukuta katika mpaka wake na Jordan wenye lengo la kuukinga uwanja mpya wa ndege wa Ramon mjini Timna dhidi ya mashambulizi ya wavamizi. Wizara ya Ulinzi ya Israel imesema ukuta huo wenye umbali wa kilomita 4.5 una kimo cha hadi mita 30 ili kuzilinda ndege zinazotua au zinazoruka kutoka katika uwanja huo dhidi ya matishio ya mara kwa mara. Akitoa taarifa ya kukamilika kwa ujenzi huo ambao ni sehemu ya mikakati ya taifa hilo ya kuimarisha ulinzi wa mipaka yake, waziri wa Ulinzi Bw Avidor Liberman amesema dola za marekani milioni 85 zimetumika kujenga ukuta huo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako